Chedieli Yohane Mgonja’s biography, net worth, fact, career, awards and life story

Intro Tanzanian politician (1934-2009)
Was Politician 
From Tanzania 
Type Politics 
Gender male
Birth 1934
Death 2009
(aged 75 years)

Chedieli Yohane Mgonja (1934-2009) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania.

HISTORIA YA CHEDIELI YOHANE MGONJA

Kuzaliwa

kuzaliwa 31 Desemba 1934, Vudee Same-Magharibi(Wilaya ya Pare)

Elimu

shule ya msingi Vudee, sekondari Ilboru na Tabora.

1959 —Chuo Kikuu Makerere.

1960 —Bwana Shauri Tanga.

1961 — miongoni mwa Watanganyika sita waliotunukiwa zawadi kwa kushiriki ktk shindano la utenzi wa wimbo wa taifa wa Tanganyika.

1961 — 62 Chuo Kikuu Cambridge UK — kozi ya utawala na Diplomasia. Wengine katika kozi hiyo ni walioapata kuwa mabalozi George Nhigula,John Malecela, Bernard Mulokozi, Raphael Lukindo, Akili Daniel.

1962 — Ubalozi wa Tanganyika New York.

1964 — kuomba kurudi nyumbani kwa nia ya kugombea Ubunge.

1965 — kupigania ubunge wilaya ya Pare vs Naibu Waziri na katibu mwenezi wa Tanu Elias Kisenge.

1965 — 67 Mbunge wilaya ya Pare, Waziri wa Maendeleo na Utamaduni. rekodi ya kuwa waziri kijana kuliko wote Tanzania.

1967 — 68 Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi ( Mambo ya Nje ). Waziri wa kwanza kujiunga na mafunzo ya JKT. Baadaye kuendelea na mafunzo ya mgambo. Waziri aliyetoa tamko la serikali ya Tanzania kuitambua Jamhuri ya watu wa Biafra.

1968 — 72 Waziri wa Elimu. Mabadiliko makubwa katika mfumo wetu wa elimu yalifanyika kipindi cha uongozi wake.

1972 — 75 Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Chama Mtwara. Ni uteuzi pekee ambao Mwalimu alimjulisha kabla haujatangazwa. Ilikuwa ni kipindi cha madaraka mikoani na vita ya ukombozi ya Msumbiji. Mkoa wa Mtwara kushika nafasi ya pili, ukifuatia Dar es Salaam, katika kuchangia vita vya ukombozi.

1977 — Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Chama Tabora.

1977 — 1980 Waziri wa Utamaduni, Vijana, na Michezo. Tanzania kukataa shinikizo la Marekani kususia michezo ya Olimpia mjini Moscow. Ujumbe wa Marekani uliletwa na Mohamed Ali.

1980 — 1982 kushinda Ubunge. Kushinda kesi dhidi yake mahakama Kuu Arusha. Kuvuliwa Ubunge na mahakama ya Rufaa Tanzania.

1984 — kuteuliwa na Raisi Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

1985 — 95 Mbunge Wilaya ya Same: vs Jonas Manento (85) vs. Dr.Kivurunya Mtera (90).

SIASA

Alikuwa Waziri wa Elimu, Habari na Michezo, na Waziri wa nchi mambo ya nje. Aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara na Tabora. Aliingia kwenye siasa mwaka 1965, akiwa Mbunge wa Upare/Same na mwaka huo huo akateuliwa kuwa waziri wa utamaduni, siasa na michezo.

Mgonja alikuwa kwenye siasa mpaka mwaka 1995, ambapo wakati wote alikuwa akiliwakilisha wilaya ya Same.

Mgonja aliongoza wizara mbalimbali katika Serikali ya awamu ya kwanza.

==Mafanikio ya Mgonja Katika Wilaya yake ya Same ==. Kwa upande wa Elimu alisisitiza ujenzi wa shule za msingi kila kata katika jimbo lake la same. Ndio maana wakati wake wasomi wengi walitoka Upareni na Kilimanjaro kwa ujumla.

Ujenzi wa Miundo Mbinu: Wilaya ya Same ina milima mingi sana, lakini pamoja na milima hiyo wananchi wa Same chini ya uongozi wa ndugu Mgonja waliweza kuchonga bara bara kwenye miteremko hiyo mikali, kwa kutumia falsafa ambayo Wapare wanaita “MSARAGAMBO” ambapo Mwalimu Nyerere alipotembelea Vudee na kuona kazi nzuri ya ujenzi wa barabara iliyofanywa na wananchi wa Same hasa Vudee aliwaita “Wachina” wa Tanzania.

KESI YA UCHAGUZI YA CHEDIELI YOHANE MGONJA

Katika uchaguzi wa mwaka 1980 Mgonja alishitakiwa kwenye kesi ya uchaguzi kuwa aliiba kura za uchaguzi (election irregularities) na kwa hiyo ushindi wake wa ubunge hakuwa halali.

1980 — 1982 kushinda Ubunge. Kushinda kesi dhidi yake mahakama Kuu Arusha. Kuvuliwa Ubunge na mahakama ya Rufaa Tanzania.Mahakama ya rufaa ya Tanzania ilimhukumu Mgonja kutoshiriki siasa/uchaguzi kwa kipindi cha miaka 10 katika kesi ya uchaguzi ya miaka ya 80.

Mwaka 1983 Kuteuliwa na Mwalimu J.K.Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Mwalimu akamteua Mgonja kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kabla ya kumalizika adhabu yake. Mwanasheria Mkuu wa wakati ule Joseph Sinde Warioba alimshauri mwalimu kuwa suala hilo lingeleta mgogoro wa Kikatiba bungeni. Kwa hiyo Waziri Mkuu Sokoine alimshauri Mwalimu na kutengua uteuzi wake.

Kabla Mwalimu Nyerere hajaondoka madarakani alimpunguzia Mgonja adhabu yake. Mgonja aligombea ubunge wa Same katika uchaguzi wa mwaka 1985, wananchi wa Same walimpa ushindi Mgonja. Katika uchaguzi wa mwaka 1990, wananchi wa Same, walimrudisha bungeni tena kipenzi chao Chedieli Yohane Mgonja “Kaghembe”.

Na mwaka 1995 ukawa mwisho wake wa kushiriki siasa.

KUFARIKI

Alifariki tarehe 30 Januari 2009, kwa ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu jijini Dar es salaam. Mke wake anaitwa Lilian Mgonja na bado yuko hai kijijini kwake Vudee Same Magharibi. Mgonja alikuwa ni mkazi wa kijiji cha Vudee Same Kilimanjaro.

MWANDISHI WA KITABU

Ameandika Kitabu kinachoitwa “JOHARI YA MAISHA YANGU”.

You May Also Like

Ezra Miller’s net worth, biography, fact, career, awards and life story

Ezra Miller Net Worth: Ezra Miller is an American actor who has a net worth of $3 million dollars. Born September 30, 1992 in Wyckoff, New Jersey, he gained early attention for his roles as Vincent “Vinnie” Rizzo, Jr. in City Island (2009), as Elliot Hellman in Another Happy Day (2011) and in the title role of We Need to Talk About Kevin (2011). He also starred in the teen drama The Perks of Being a Wallflower (2012), a role which was just the departure from his former roles that he needed to establish himself as an actor who could potentially fit a variety of roles. Miller began performing on stage at the age of six, landing a role in the U.S. premiere of Philip Glass’ contemporary opera White Raven and was a member of New York’s Metropolitan Opera Children’s Chorus. Training for opera at such a young age helped Miller overcome a speech impediment. At age 16, Miller dropped out of The Hudson School in New Jersey to pursue acting. In 2008, he appeared in Afterschool, his film debut in which he starred as an Internet-addicted student who records (on video) two girls overdosing on drugs. That same year, Miller was cast on the hit series Californication on Showtime. He built up his résumé with guest appearances on Law & Order: Special Victims Unit and with an appearance in the independent comedy City Island (2009). He also had roles in the 2010 films Beware the Gonzo and Every Day, as a gay teenager whose parents struggle with an unexpected romantic crisis. On June 28, 2011, in Pittsburgh, Pennsylvania, Miller was a passenger in a vehicle that was pulled over for a broken brake light, and police discovered that Miller had 20 grams of marijuana in his possession. He was initially charged with drug possession, but the charge was later dropped by a judge. Miller instead faced a penalty of $600 for two citations of disorderly conduct.
Read More