Blandina Changula’s biography, fact, career, awards, net worth and life story

Intro Tanzanian actress
Is Actor
From Tanzania
Type Film, TV, Stage & Radio
Gender female
Birth

27 July 1983

Age 37 years
Star sign Leo

Blandina Changula (amezaliwa tar. 27 Julai 1983 mkoani Shinyanga, Tanzania ni muigizaji wa vipindi vya telesheni na filamu nchini Tanzania.

Maisha ya Mwanzo

Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.

Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo shule ambayo alimalizia kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.

Blandina Changula anatokea kundi la Kaole Sanaa Group, ni kundi ambalo linafahamika sana nchini Tanzania kwa kutoa nyota wengi wa uigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota
hao, wengine ni Steven Kanumba, Vincent Kigosi (Mr Ray), Tea na wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa Group.
Kwa hivi sasa Blandina Chagula kwa kushirikiana na msanii mwenzake Vincent Kigosi wana kampuni yao pamoja iitwayo RJ Company (Ray & Johari coumpany ) ambayo inafanya kazi ya kuzalisha filamu mbalimbali kama vile Bed Rest, Bad Luck , Wrong hope , Peace of mind , Fair Decision nk.

Baadhi ya Filamu Alizoigiza

  • Sikitiko Langu
  • Johari 1 na 2
  • Dangerous Desire
  • Dar 2 Lagos

Anaoshirikiana Nao

  • Steven Kanumba
  • Vincent Kigosi
  • Muhsein Awadh
  • Ally Chaowa
  • Kulwa Kikumba
  • Mwanaidi Suka
  • Nuru Nassoro
  • Ndumbagwe Misayo
  • Donah Redson
  • Fatuma Makongoro
  • Emmanuel Myamba
  • Charles Magari
  • Fatuma Mvura
  • Mohamed Mwikongi
  • Fadhili Omar

Wanigeria

  • Mercy Johson
  • Nkilu Sylvanus
  • Nancy Okeke
  • Bimbo Ankintola
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Blandina Changula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
You May Also Like